Kamati yatoa maelekezo miradi iliyokwama

KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii, imeitaka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wanawake na Makundi Maalumu kuunga mkono kwa kutoa fedha ili kukamilisha miradi inayoendelea kutekelezwa katika Taasisi ya Ustawi wa Jamii (ISW) ikiwemo mradi wa ujenzi wa ukumbi.

Akizungumza wakati kamati hiyo ilipotembelea taasisi hiyo leo jijini Dar es Salaam na kukagua mradi huo unaojengwa kwa mapato ya ndani, Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Dk Regina Malima amesema wanaipongeza taasisi hiyo kwani mbali na majukumu yake ya kitaaluma, imeonesha jitihada kubwa katika kushirikiana na jamii kwa kutoa elimu na uwezeshaji katika nyanja mbalimbali.

Amesema mradi huo unahitajika kuangaliwa kwa haraka na maboresho yanahitajika ili kuhakikisha jengo hilo linakuwa rafiki kwa watu wote, ikiwemo wenye ulemavu kwani kutofanya hivyo kutakuwa ni kinyume na azma ya usawa katika elimu.

“Vilevile tumeshuhudia dhamira ya wajumbe wa kamati na wabunge wote ya kuhakikisha wizara inaingilia kati pale ambapo taasisi inakosa uwezo wa kutekeleza baadhi ya majukumu.

“Miradi inayotekelezwa inaonekana kuchukua muda mrefu, huku rasilimali nyingi zikielekezwa kwenye tafiti na shughuli za kitaaluma. Hivyo ni muhimu kuwepo kwa majadiliano ya kitaifa ili kupata suluhisho la pamoja litakaloinua viwango vya elimu,” amesema.

Amesema hadi sasa ujenzi huo umefikia zaidi ya asilimia 80, jambo ambalo ni la kupongezwa sana ambapo  kukamilika kwa jengo hili kutaboresha mazingira ya kujifunzia kwa wanafunzi na kuongeza ubora wa huduma za elimu zinazotolewa na taasisi hii.

Pamoja na mafanikio hayo, kama Kamati pia  imetoa ushauri kwa taasisi hiyo kuhakikisha kuwa miundombinu inazingatia mahitaji ya makundi yote, hususan watu wenye ulemavu ili kutoa fursa sawa kwa wanafunzi wote.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dk John Jingu amesema watafanya tathmini ya kina   katika taasisi zote kwa ujumla, lengo ni kubaini maeneo yenye upungufu ili tuyaboreshe na kuimarisha madawati haya yaweze kufanya kazi kwa ufanisi zaidi.

“Jambo lingine ni kuhusu bajeti hasa katika kusaidia ukamilishaji wa jengo letu pamoja na miundombinu mingine ikiwemo nyumba za watumishi, makazi katika maeneo kama Ngerengere tunatamani kuona mazingira bora ya makazi kwa watumishi utekelezaji wake unategemea ukomo wa bajeti uliopo,”amesema.

Mkuu wa Chuo cha Ustawi wa Jamii Dk Joyce Nyoni amesema gharama za ujenzi wa mradi huu ni Sh milioni 666.4, ambapo chanzo cha mapato ni ya ndani ya taasisi na unatarajiwa kukamilika tarehe 31 Mei, 2025.

Habari Zifananazo

3 Comments

  1. I just came across this amazing way to earn $6,000-$8,000 a week online! No selling, no struggle—just a simple system that anyone can follow. Mia Westbrook did it, and so can you! Don’t miss out on this life-changing opportunity.
    Follow Here …………… http://www.giftpay7.vip

  2. JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 12000-16700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
    .
    This is my main concern…………………… http://Www.Cash54.Com

  3. I just came across this amazing way to earn $11,000-$15,000 a month online! No selling, no struggle—just a simple system that anyone can follow. Mia Westbrook did it, and so can you! Don’t miss out on this life-changing opportunity.
    .
    This is what I do…………………… http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button