Kampuni ya Kaspesky kupigwa stop Marekani

NEW YORK, Marekani: Marekani imetangaza mpango wake wa kupiga marufuku uuzaji wa programu ya antivirus iliyotengenezwa na kampuni ya Urusi ya Kaspersky kutokana na madai ya kuwa ina uhusiano na Kremlin.

Kwa mujibu wa Waziri wa Biashara, Gina Raimondo amesema uamuzi huu umekuja baada ya kuwepo kwa ushawishi wa Moscow kuhusu kampuni hiyo kudaiwa kuwa hatari kwa miundombinu na huduma za Marekani.

Gina amesema Marekani imelazimika kuchukua hatua hiyo kutokana na uwezo wa Urusi una nia ya kukusanya na kushambulia taarifa binafsi za Wamarekani.

“Kaspersky haitaweza tena kuuza program zake Marekani au kuweka maboresho kwenye programu ambayo tayari inatumika,” Wizara ya Biashara imesema.

Hatahivyo Kampuni ya Kaspersky imesema itachukua hatua za makusudi za kisheria, ili kupinga hatua hiyo na kukana kuhusika na tuhuma hizo za kutishia usalama wa Marekani.

Hivi sasa Kampuni ya Kaspesky ambayo makao makuu yako Moscow nchini Urusi, inamiliki ofisi katika nchi 31 duniani na kuwahudumia zaidi ya watumiaji Milioni 400 na wateja wa kampuni 270,000 katika zaidi ya nchi 200.

Habari Zifananazo

Back to top button