Kampuni yapewa tuzo kwa mchango wake kwa jamii

MANYARA: CHUO cha Ukamanda na Unadhimu (CSC) Duluti mkoani Arusha, kimeipa tuzo maalumu Kampuni ya Mati Super Brands Limited inayozalisha vinywaji changamshi ya mjini Babati mkoani Manyara kwa kutambua mchango wa kampuni hiyo katika kusaidia jamii inayowazunguka.

Tuzo hiyo pia ni kutambua mchango wa kampuni hiyo katika kushirikiana vyema na taasisi mbalimbali za serikali katika shughuli za maendeleo.

Tukio hilo lilifanyika mwishoni mwa wiki mkoani humo baada ya Mwakilishi wa Mkuu wa Chuo cha Ukamanda na Unadhimu (CSC) Kanali Verus Chrysostom aliyeambatana na maofisi wengine wa ngazi za juu wa kijeshi kutoka mataifa mbalimbali kufanya ziara maalumu ya kimafunzo kwenye kampuni hiyo.

Kanali Chrysostom alisema kampuni hiyo imekuwa ikitoa fursa wa mafunzo kwa vitendo kwa maofisa wa kijeshi kwa masuala mbalimbali ikiwemo usalama wa chakula.

SOMA: NBC yatunukiwa Tuzo ya Uwajibikaji Bora kwa Jamii

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mati Super Brands Limited, David Mulokozi alikishukuru chuo hicho cha kijeshi kwa kutambua mchango wa kampuni hiyo katika masuala mbalimbali ikiwemo kurudisha sehemu ya faida wanayoipata kwa jamii inayowazunguka.

Mulokozi alisema tuzo hiyo inawapa chachu ya kuendelea kufanya vizuri kwa kushirikiana na taasisi za umma na jamii pamoja na kuzalisha bidhaa zinazozingatia ubora na usalama wa mtumiaji.

Habari Zifananazo

Back to top button