Kanuni kuboreshwa utaratibu kuthibitisha Makamu wa Rais

DODOMA; Kamati ya Kanuni za Bunge imewasilisha mapendekezo ya maboresho ya Kanuni za Kudumu za Bunge, ikiwemo kuweka kanuni mahususi inayoeleza utaratibu wa Bunge kuthibitisha uteuzi wa Makamu wa Rais inapotokea ameteuliwa baada ya kipindi cha uchaguzi kupita.

Akiwasilisha taarifa ya Kamati ya Bunge ya Kanuni za Bunge kuhusu Marekebisho au mabadiliko katika Kanuni za Kudumu za Bunge Toleo la Februari 2023, Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, ambaye pia ni Naibu Spika, Mussa Azzan, amesema:

“Kanuni zinazopendekezwa kufanyiwa marekebisho zilipitishwa na Bunge mwezi Juni, 2020. Kanuni hizo zilirekebishwa katika Nyongeza ya Nane ya Kanuni mwaka 2023, hivyo Toleo la Februari, 2023 lilichapishwa. Kanuni hizo zilianza kutumiwa rasmi na Bunge hili la Kumi na Mbili.

“Kwa kuwa Bunge hili linaelekea mwisho wa kipindi cha uhai wake, imeonekana ni muhimu kuzipitia kanuni hizi kwa lengo la kuziboresha ili zitumike wakati wa Bunge la Kumi na Tatu litakaloanza Novemba, 2025.

“Utaratibu huu ni wa kibunge na huzingatiwa na mabunge mengine ya Jumuiya za Madola,” amesema na kuongeza kuwa:

“Mheshimiwa Spika, Inapendekezwa kuwa na kanuni mahsusi inayoeleza utaratibu wa Bunge wa kuthibitisha uteuzi wa Makamu wa Rais pale inapotokea ameteuliwa baada ya kipindi cha uchaguzi kupita (Ibara ya 50(4) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977).

“Utaratibu unaopendekezwa unatokana na uzoefu wa Bunge letu kuendesha mchakato kama huo,” amesema Makamu Mwenyekiti.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button