Kapinga ataka kasi ya Kuunganisha Umeme vijijini

DODOMA: WAZIRI wa Nishati, Judith Kapinga amewaagiza Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kuongeza kasi ya kuwaunganishia umeme wananchi vijijini katika maeneo ambayo tayari yamefikiwa na miradi ya usambazaji umeme ili miradi hiyo iweze kuwa na tija.

Amiagiza hayo akiwa jijini Dodoma wakati wa kikao chake na Uongozi wa REA kilicholenga kupata  taarifa za utekelezaji wa Miradi ya Nishati Vijijini na mipango iliyopo  katika utekelezaji wa miradi hiyo.

“Haipendezi kuona mradi umefika katika kijiji na umekamilika lakini unakuta kaya tano au kumi tu zimeunganishwa, hii hailingani na nguvu iliyotumika kuufikisha mradi huo katika Kijiji husika, hivyo angalieni upya namna bora ya kuwahamasisha wananchi ili wajiunge na huduma hii,” amesisitiza Kapinga.

Amewasisitiza kuwa, suala la kuunganisha wateja walichukue kwa uzito mkubwa kama  wanavyosimamia  upelekaji wa umeme katika  Vijiji na hii italeta  matokeo chanya ya utekelezaji wa miradi hiyo.

“Tumieni njia mbalimbali katika kuwafikia wananchi ikiwemo kuungana nao katika mikusanyiko ya tamaduni zao za asili kama vile kwenye ngoma na sehemu nyingine kama hizo kulingana na maeneo husika na waelezeni ukweli kuwa gharama za kuunganisha umeme vijijini ni shilingi 27,000 ili waone njia bora ya kupata hizo fedha ili waweze kuunganishiwa umeme”, amesema Kapinga.

Aidha, ameielekeza REA kuwajengea uwezo Wasimamizi wa Miradi ya Umeme Vijijini ili waifahamu ipasavyo miradi hiyo na hivyo waongeze ufanisi katika kuwasimamia vyema Wakandarasi wanaotekeleza miradi husika.

Amesema kuwa, wasimamizi hao wanatakiwa kufahamu maeneo ya miradi yao na waanze kazi ya ufuatiliaji wa utekelezaji wa miradi kuanzia pale ambapo Serikali inatoa fedha na kama kuna changamoto ama vikwazo vyovyote waweze kuvishughulikia mapema.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mhandisi Hassan Saidy amemueleza Naibu Waziri huyo kuhusu utekelezaji wa Miradi ya Nishati Vijijini iliyotekelezwa na inayotarajiwa kutekelezwa ambapo amemueleza Mhe. Kapinga kuwa, REA imepokea maelekezo aliyotoa kwa utekelezaji ili kuzidi kuboresha Sekta ya Nishati vijijini.

Kikao hicho pia kimehudhuriwa na Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati, Athumani Mbuttuka na Viongozi wengine Waandamizi kutoka Wizara ya Nishati na REA.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
8 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
NYUMBA MIJINI NA VIJINI
NYUMBA MIJINI NA VIJINI
23 days ago

TANGAZO

KAMPUNI YA WOTE COMPANY LIMITED INAWATANGAZIA VIJANA WA TANZANIA AJIRA 1 KWA MTANZANIA ATAKAE SAMBAZA UFISADI/WIZI/UHARIBIFU KWENYE KILA NYUMBA MIJINI NA VIJINI

Capture.JPG
Marie Allen
Marie Allen
Reply to  NYUMBA MIJINI NA VIJINI
23 days ago

I get paid more than $140 to $170 per hour for working online. I heard about this job 3 months ago and after joining this (Qn)I have earned easily $25k from this without having online working skills . Simply give it a shot on the accompanying site…
.
.
.
Here is I started.…………>> http://Www.Smartcareer1.com

NYUMBA MIJINI NA VIJINI
NYUMBA MIJINI NA VIJINI
23 days ago

TANGAZO

KAMPUNI YA WOTE COMPANY LIMITED INAWATANGAZIA VIJANA WA TANZANIA AJIRA 1 KWA MTANZANIA ATAKAE SAMBAZA UFISADI/WIZI/UHARIBIFU KWENYE KILA NYUMBA MIJINI NA VIJINI..

Capture.JPG
NYUMBA MIJINI NA VIJINI
NYUMBA MIJINI NA VIJINI
23 days ago

TANGAZO

KAMPUNI YA WOTE COMPANY LIMITED INAWATANGAZIA VIJANA WA TANZANIA AJIRA 1 KWA MTANZANIA ATAKAE SAMBAZA UFISADI/WIZI/UHARIBIFU KWENYE KILA NYUMBA MIJINI NA VIJINI

PAMBANA NA UMASIKINI

Capture.JPG
NYUMBA MIJINI NA VIJINI
NYUMBA MIJINI NA VIJINI
23 days ago
babofe8659
23 days ago

JOIN US I’m making a good salary from home 16580-47065/ Doller week , which is amazing under a year ago I was jobless in a horrible economy. I thank God every day I was blessed with these instructions and now it’s my duty to pay it forward and share it with Everyone,
Here is I started.…………> http://profitguru7.com

NYUMBA MIJINI NA VIJINI
NYUMBA MIJINI NA VIJINI
Reply to  babofe8659
23 days ago

Grow very Fast Kids… so that you will be like them…..

https://www.facebook.com/reel/1048183376369136

Nanetteoho
Nanetteoho
23 days ago

I’ve gained only within four weeks by comfortably working part-time from home. Immediately when I had lost my last business, mtg I was very troubled and thankfully
following website___________ http://Www.Careers12.com

Last edited 23 days ago by Nanetteoho
Back to top button
8
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x