Kasekenya aipa TANROADS miezi miwili.

NAIBU Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya, ameiangiza Wakala wa Barabara (TANROADS), Mkoa wa Tabora kuhakikisha wanasimamia ipasavyo ukarabati na uboreshaji wa kiwanja cha ndege cha Tabora ili kikamilike ifikapo Machi 2024.

Kasekenya ameyasema hayo mara baada ya kukagua kiwanja hicho na kutoridhishwa na kasi ya ujenzi wake, ambapo mradi huo.

Kwa upande wake, Mhandisi Mkazi anayesimamia mradi huo, Mhandisi  Vicent Aron amesema kwa kuzingatia shughuli zote ambazo zimefanyika kwenye ujenzi, mradi kwa sasa umefika asilimia 12.9 dhidi ya maendeleo yaliyopangwa ya asilimia 13 kwa kuzingatia siku 75 zilizotumika.

Aidha, ameongeza kuwa wameongeza jitihada za kumsimamia Mkandarasi M/S BEIJING CONSTRUCTION ENGINEERING GROUP CO.LTD, katika kuhakikisha anamaliza kazi kwa wakati kwa kuongeza idadi ya wafanyakazi, kuongeza muda wa kufanya kazi siku zote za wiki na sikukuu za kimataifa.

Meneja wa Wakala wa Barabara Nchini (TANRODAS) Mkoa wa Tabora, Mhandisi Raphael Mlimaji amemuhakikishia Naibu Waziri wa Ujenzi Mhandisi Godfrey Kasekenya kusimamia kiwanja cha ndege hicho kwa ukaribu na kuhakikisha kinakamilika kwa muda ulipangwa.

Kwa upande wa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Balozi, Dk Batlida Salha Burian, ameishukuru Serikali ya awamu ya sita kupitia Wizara ya Ujenzi, kwa uboreshaji wa Kiwanja cha ndege, kwani kukamilika kwake kutatochechea shughuli za kiuchumi na kimaendeleo katika mkoa huo.

Habari Zifananazo

Back to top button