Kasekenya mambo safi Ileje

SONGWE: ALIYEKUWA Naibu Waziri wa Ujenzi na Mbunge wa Jimbo la Ileje, Mhandisi Godfrey Kasekenya ameongoza kura za maoni kwa kupata kura 5102.
Akitangaza matokeo hayo leo Agosti 5,2025 katibu wa chama chaMapinduzi wilaya ya Ileje Hassan Yusuph Lyamba amesema matokeo hayo yametokana na wajumbe kupiga kura Agosti 4,2025.
Lyamba amesema Mhandisi Godfrey Kasekenya aliyekuwa akitetea nafasi yake ikiwa ni awamu ya pili katika Jimbo hilo ameongoza katika kura hizo kwa kupata kura 5102 akifuatiwa na Stella Fiyao aliyepata kura 1035 ambaye alihamia akitokea Chama cha Demkokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambapo alikuwa Mbunge wa viti Maalum katika bunge lililopita
Amewataja wengine na idadi ya kura kuwa ni Joel Kaminyoge(275), Elius Ndabila(224), Edisoni Ngabo(184), Ezekiel Kibona(144) na Claudia Kita(95).

