Kasore: vijana changamkieni fursa za ufundi

MAMLAKA ya Elimu ya Mafunzo na Ufundi Stadi (VETA) imewataka  vijana wa kitanzania kutumia fursa ya mafunzo ya ufundi stadi kujiajiri   na kuleta mapinduzi ya viwanda nchini.
Hayo ameseyasema Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa VETA CPA Anthony Kasore wakati akizungumza na Waandishi wa Habari katika Banda la VETA kwenye maonesho 47 ya Biashara Kimataifa Dar es Salaam (DITF) yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Sabasaba Jijini Dar es Salaam.
Kasore, amesema kuwa serikali imewekeza nguvu katika ujenzi wa vyuo mafunzo ya ufundi stadi katika kuhakikisha vijana wanapata ujuzi wa kuweza kuajiriwa na kujiajiri pasipo kuwepo kwa changamoto.
Amesema VETA inatarajia kujenga vyuo 64 ikiwemo kimoja cha Mkoa wa Songwe na vingine vyote vya wilaya.
Aidha, amesema serikali ya awamu ya sita ya Rais Samia Suluhu Hassan iko bega kwa bega na VETA katika kuwapatia vijana ujuzi waweze kutengeneza ajira na maendeleo kwa ujumla.
Kasore amesema katika utoaji wa mafunzo kumekuwa na ubunifu ambapo wabunifu walimu na wanafunzi kazi ya VETA ni kuwashika mkono kwa kuwa na miliki ili watu wengine wasije wakazifanyia biashara.
Kasore amesema wenye viwanda na wawekezaji wasipate changamoto ya nguvu kazi kutokana na nguvu kazi hiyo imeshazalishwa na VETA.
Amesesma VETA inashirikiana na Costech katika kuhakikisha wabunifu wanakuwa wanatambuliwa na kuweza bunifu hizo kwenda mbali zaidi.