Madiwani Mikindani wamchagua meya mpya

MTWARA: HALMASHAURI ya Manispaa ya Mtwara Mikindani mkoani Mtwara imefanya uchaguzi wa meya na naibu meya ambapo diwani wa kata Jangwani, Saidi Zaidi ameibuka mshindi katika nafasi ya umeya kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM).

Hayo yamejiri leo Disemba 4, 2025 wakati wa mkutano wa kwanza wa Baraza la Madiwani la manispaa hiyo uliyofanyika kwenye manispaa hiyo.

Aidha, baraza hilo mbali na kufanyika kwa uchaguzi huo lakini limehusisha kiapo cha madiwani hao, uundaji wa kamati za kudumu za halmshauri, kupokea taarifa ya utekelezaji wa shughuli za halmashauri zilizofanyika katika kipindi ambacho baraza la madiwani lilivunjwa na mengine.

Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Katibu Tawala wa Wilaya hiyo Richard Mwalingo amesema idadi ya wapiga kura ilikuwa 24 hivyo amemtangaza Said Zaid kuwa mshindi wa kura zote zilizopigwa kutokana hakuna kura iliyoharibika wala hapana.

Nafasi nyingine ni naibu meya iliyogombewa na diwani wa kata Majengo, Sixmund Lungu aliyetetea kitu chake hicho kwa kipindi kingine tena aliyeibuka na ushindi wa kura zote kutokana na idadi ya wapiga kura hao kwani hakuna kura iliyoharibika wala hapana.

Akitoa shukrani kwa wapiga kura hao, meya huyo wa manispaa hiyo “Niwashukuru sana wajumbe kwa kuniamini na kunichagua kwa kura nyingi na naahidi kutekeleza majukumu haya kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizopangwa kikubwa naomba ushirikano”

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mtwara Mjini, Salum Naida amesema wananchi wa mtwara mjini wamewachagua madiwani hao kutokana na kukiamini chama kwani hilo ni deni kubwa kwa wananchi hivyo wakawatumikie kikamilifu.

Habari Zifananazo

2 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button