Katiba mpya ni suala la muda-Rais Samia

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema muda sio mrefu ataunda kamati kwa kushirikiana na vyama vingine vya siasa ambayo itashughulika na suala la katiba mpya.

Akizungumza leo Machi 8, 2023 kwenye Kongamano la Siku ya Wanawake Duniani wa Chadema, Rais Samia amesema suala hilo hakuna anayelipinga.

“Swala katiba hakuna anayekataa hata chama changu hakuna anayekataa, na muda si mrefu tutatangaza kamati ambayo itashughulikia jambo hilo”.

amesema Rais Samia.

Kiongozi huyo wa nchi amesema kuwa “Hakuna kisichowezekana kwa mazungumzo, tulishuhudia nchi kadhaa ziliingia kwenye vita hakukupatikana suluhu, lakini suluhu ikaja kupatikana kwa mazungumzo”.

Habari Zifananazo

Back to top button