UN yaonya kuhusu ghasia Gaza

NEW YORK : KATIBU Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres amesema amani ya kudumu katika Ukanda wa Gaza haiwezi kupatikana endapo ghasia zitaendelea. Amesema ili kufanikisha amani, kunahitajika mshikamano wa kidiplomasia, utiifu wa sheria za kimataifa na kuheshimu utu wa binadamu.

Kwa upande wake, msemaji wa ulinzi wa raia katika eneo hilo amesema Wapalestina 15 wamefariki dunia baada ya majeshi ya Israel kushambulia nyumba na mahema katika mji wa Gaza City. Viongozi mbalimbali wa kimataifa waliokutana katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa wameeleza masikitiko yao na kutoa mapendekezo ya namna ya kumaliza vita vya Israel na Palestina.

Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron amesema ikiwa Rais wa Marekani, Donald Trump, anataka kushinda Tuzo ya Amani ya Nobel, basi hana budi kushinikiza Israel kumaliza vita hivyo, akisema ndiye pekee mwenye ushawishi wa kutosha.

Naye Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza, Yvette Cooper, amesema hatua za kijeshi za Israel zimezidisha hali mbaya ya kibinadamu Gaza na kufanya iwe vigumu kuwakomboa mateka wa Israel wanaoshikiliwa.

Hata hivyo, Marekani imekosoa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kufuatia uamuzi wa baadhi ya nchi za Magharibi kulitambua taifa la Palestina. Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa, Mike Waltz, amesema mkutano ulioitishwa na Ufaransa na Saudi Arabia Jumatatu, ulikuwa wa kiutendaji pekee.

Mkutano huo ulilenga kuhimiza kupatikana suluhisho la serikali mbili moja ya Israel na nyingine ya Palestina. SOMA: Guterres asisitiza Afrika kupata uwakilishi Umoja wa Mataifa

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button