Katimba aongoza kura za maoni Kigoma

KIGOMA: Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Zainab Katimba ameongoza kura za maoni za uchaguzi wa wabunge wa Viti Maalum Mkoa Kigoma akiwania kutetea tena nafasi yake ya ubunge kupitia Viti Maalum UWT Kigoma.
Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo msimamizi wa uchaguzi ambaye ni Mkuu wa Mkoa Mara, Kanali Evance Mtambi amesema kuwa Katimba aliongoza kwa kupata kura 973 kati ya kura halali 1056 zilizopigwa ambapo jumla ya kura zote zilizzopigwa zilikuwa 1065 na kura tisa ziliharibika.
SOMA ZAIDI
Nafasi ya pili ilichukuliwa na Naomi Mwaipopo aliyepata kura 686 ambazo zinampata nafasi pia ya kuteuliwa kuwa mbunge wa Viti Maalum kutoka Kigoma ambapo Mwenyekiti staafu wa UWT Mkoa Kigoma, Selina Makabe alishika nafasi ya tatu kwa kupata kura 176.
Mtambi alimtangaza Ashura Kahoye aliyepata kura 89, Amina Kaumo kura 80, Sabrina Sungura alipata kura 71, Jackline Rugo na Prisca Mapunda alipata kura 20.

