Kaya elfu tatu zakimbia makazi Sudan

SUDAN : SHIRIKA la Uhamiaji la Umoja wa Mataifa (IOM) limetangaza kuwa maelfu ya watu wameukimbia mji wa Um Rawaba nchini Sudan baada ya kuzuka mapigano wiki iliyopita kati ya jeshi la Sudan na wanamgambo wa RSF.

Kwa mujibu wa IOM, watu kutoka kaya 1,000 hadi 3,000 walilazimika kuukimbia mji wa Um Rawaba, ulio katika jimbo la Kordofan Kaskazini, kusini mwa Sudan, katika kipindi cha siku tano.

IOM imesema zaidi ya watu 250,000 wamekimbia makazi yao kutokana na kuongezeka kwa hali ya wasiwasi wa usalama, huku mapigano yakiendelea katika eneo la Kordofan.

Advertisement

Kwa sasa, zaidi ya milioni 11.5 za watu nchini Sudan wamekuwa wakimbizi wa ndani, ikiwa ni pamoja na milioni 2.7 walikimbia makazi yao kutokana na migogoro ya awali.

Umoja wa Mataifa umeutaja mzozo wa wakimbizi wa Sudan kuwa ni miongoni mwa migogoro mikubwa zaidi duniani kwa sasa. SOMA: SUDAN: Tom Fletcher ataka hatua za haraka kukabiliana na mzozo