Kenya yapinga mauaji wanawake

KENYA : POLISI nchini Kenya wametumia mabomu ya machozi kuwatawanya waandamanaji waliokusanyika kuandamana kupinga ongezeko la matukio ya mauaji ya wanawake nchini humo.
Takribani watu watatu wamekamatwa, huku waandamanaji wengine wakidai kuwa polisi ilipinga kufanya maandamano.
“Tuliomba kibali lakini mamlaka ilizuia kufanyika kwa maandamano,” mratibu wa maandamano Njeri Migwi alisema.
Mnamo Novemba, Rais William Ruto alisema serikali yake imejitolea kushughulikia matukio hayo yanayoongezeka, na aliahidi dola 800,000 kwenye kampeni iliyoitwa “Nyumba Salama, Nafasi Salama”.
Januari mwaka huu, waandamanaji hao walifanya maandamano kama hayo ya amani na kuidhinishwa na mamlaka. SOMA: Asilimia 40 ya wanawake wamefanyiwa ukatili
Waandamanaji hao wametoa wito maalum wa kukomesha ongezeko la unyanyasaji dhidi ya wanawake pamoja na sheria kali zichukuliwe dhidi ya wahalifu.
Kesi zipatazo 97 za mauaji ya wanawake zimeripotiwa katika vituo vya polisi nchini humo katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita.



