Kiapo wahitimu mitihani ya TNMC

DODOMA: Jumla ya wauguzi na wakunga wapya 2099 waliofaulu Mtihani wa Baraza la Uuguzi na Ukunga (TNMC), uliofanyika 29/12/2023 ili kupata sifa za kuorodheshwa, kusajiliwa na kupewa leseni za kutambuliwa rasmi kama wataalamu wa kada ya uuguzi na ukunga hapa nchini, wamekula kiapo cha kuitumikia taaluma hiyo kwa kuzingatia, maadili, miiko, sheria na kanuni za uuguzi na ukunga.

Kati ya wahitimu hao 346 ni wahitimu wa Shahada ya kwanza, 1737 ni ngazi ya Stashahada huku 16 wakiwa ni ngazi ya Astashahada.

Mahafali hayo ya 10 ya Kitaaluma yanayoratibiwa na Baraza la Uuguzi na ukunga Tanzania (TNMC) yamefanyika Jijini Dodom huku Mgeni wa heshima akiwa Mganga Mkuu wa Serikali Dk Tumaini Nagu.

 

Habari Zifananazo

Back to top button