Kihongosi: Siasa isiingie kwenye maendeleo

MARA: KATIBU wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Kenani Kihongosi amewataka wananchi kutokuruhusu siasa kuingia katika maendeleo akiwasisitiza walinde miundombinu inayopelekwa na serikali.
Kihongosi ameeleza hayo leo Mei 16,2026 alipotembelea na kukagua mradi wa shule ya Sekondari ya Nyasariso Kata ya Bunagi Tarime Vijijini mkoani Mara, ikiwa ni muendelezo w aziara yake katika mkoa huo.

Akizungumza baada ya kukagua mradi huo Kihongosi amewasisitiza wananchi kulinda miundombinu inayopelekwa na serikali katika maeneo yao kwani yanapelekwa kwa manufaa yao wenyewe, hivyo wasiiharibu wala kuichoma kutokana na uchochezi wa kiaisasa.
Kihongosi amesema siasa ifanyike lakini isiingie katika maendeleo ya nchi, akisisitiz akuwa mtu mwelevu analinda nyumbani kwao lakini matu ambaye si mwerevu anaharibu nyumbani kwao.

Kihongosi amezungumza na kuwataka wananchi kutokuruhusu siasa kuingia katika maendeleo, akiwasisitiza walinde miundombinu na miradi ya maendeleo wanayopelekewa ikiwemo shule hiyo kwani ni kwa manufaa yao wenyewe.
“Sasa siasa isiingie kwenye maendeleo, siasa ifanyike maendeleo ya nchi yasonge mbele watu wa Tarime msipolinda miundombinu yenu hakuna wakuwalindia, shule ikichomwa maana yake watoto wote warudi nyumbaniHiyo ni hasara kwa wazazi na wananchi usika,” amesisitiza.

Akitoa taarifa fupi ya mradi huo Mkuu wa Shule ya Sekondari Nyasarisho, Paschal Sobu amesema shule hiyo ni ya mchanganyiko inavijana wa kidato cha kwanza hadi cha sita, huku kidato cha kwanza hadi cha nne ni wavulana na wasichana lakini kidato cha stano na sita ni wavulana tu.
Amesema shule hiyo imejengwa kwa kiasi cha Sh bilioni 1.6 ambayo Sh bilioni moja imetoak katika serikali kuu na zaidi ya Sh milioni 600 kutoka katika mapato ya ndani ya Halmashauri ya Tarime “Tunayo miuondombinu kama ulivyoikagua yako madarasa 13, ofisi tano, lipo jengo la utawala eneo ulilosimama, maabara za kisasa ulizoziona, ya Kemia na baolojia lakini tunabwalo la chakula, jiko la ndani ambayo yanatumia nishati safi,”amesema Sobu.



