Rais Mstaafu Kikwete ashiriki mkutano AUDA-NEPAD

Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Elimu Duniani (Global Partnership for Education – GPE) Rais Mstaafu Jakaya Kikwete ameshiriki katika Mkutano wa Ngazi ya Juu ulioandaliwa na Taasisi ya Maendeleo ya Umoja wa Afrika (AUDA-NEPAD), Addis Ababa, Ethiopia.

Mkutano huu uliohusu Mpango wa Sayansi, Teknolojia na Uvumbuzi barani Afrika (STISA 2034), ulikutanisha wadau mbalimbali barani Afrika na nje ya bara hilo kujadili mchango wa elimu, sayansi, teknolojia na uvumbuzi katika maendeleo barani humo.

Alisisitiza katika hotuba yake kuwa elimu ni msingi wa maendeleo na kuwa ni muhimu nchi wanachama wa Umoja wa Afrika ziweke kipaumbele katika kutenga rasilimali za kutosha katika sekta ya elimu kwani kufanya hivyo kutawezesha matumizi ya kisasa ya sayansi na teknolojia na hatimaye uvumbuzi kwa maendeleo ya nchi moja moja na bara la Afrika kwa ujumla.

“Elimu huwapa watu maarifa na ujuzi wa kushughulikia mahitaji na changamoto za kimaendeleo za taifa na jamii kwa ujumla…na kwamba nchi zilizoendelea zaidi, zimewekeza sana katika elimu, sayansi na teknolojia,” alisema Rais Mstaafu.

Habari Zifananazo

4 Comments

    1. I just came across this amazing way to earn $6,000-$8,000 a week online! No selling, no struggle—just a simple system that anyone can follow. Mia Westbrook did it, and so can you! Don’t miss out on this life-changing opportunity.
      .
      Follow Here ……………………… https://Www.Cash54.Com

    2. I get paid over 220 Dollars per hour working from home with 2 kids at home. i never thought i’d be able to do it but my best friend earns over 15k a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life. This is what I do, check it out by Visiting Following Website…

      .
      M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→→→→→→ https://Www.Payathome9.Com

  1. I get paid more than $120 to $130 per hour for working online. I heard about this job 3 months ago and after joining this i have earned easily $15k from this without having online working skills.
    This is what I do…..  www.join.work27.com 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button