MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Kanda ya Kaskazini imeteketeza bangi viroba vya bangi kavu 237 zikiwa na mbegu zenye uzito wa kilo 310 ambazo zilikuwa tayari kupandwa.
Akizungumza katika zoezi la kuteketeza bangi hizo dampo la Kikatiti wilayani Arumeru, mkoani Arusha, Mkuu wa oparesheni wa mamlaka hiyo Kanda ya Kaskazini, Innocent Masangula amesema bangi hizo zilikamatwa katika oparesheni maalum iliyoongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Emanuela Kaganda.
DC Kaganda amesema bangi hizo zimeteketezwa eneo hilo na katika kipindi cha Septemba gunia 90 za bangi zilikamatwa na mwezi Oktoba mwaka huu, gunia 225 na kupelekea jumla kuwa gunia 316 sanjari na kilo 310 za bangi.
“Gunia nyingine tumeziteketezwa shambani nyingine zimeteketezwa hapa,na tutaendelea na zoezi hili”
Amesema serikali imejipanga kutoa elimu juu ya madawa ya kulevya ikiwemo ulimaji wa zao mbadala ili waachane na madawa hayo