Kinana ataka mshikamano

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Abdulrahman Kinana, amewataka viongozi wa CCM Wilaya ya Kibiti mkoni Pwani kuimarisha umoja na mshikamano kwa kuwa ndio siri ya maendeleo.

Kinana, you ameyasema hayo leo Julai 15, 2025 alipozungumza na viongozi mbalimbali katika kikao cha ndani baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Ofisi Mpya ya CCM Wilaya ya Kibiti.

Amesema, mafanikio yanayoendelea kuonekana katika wilaya hiyo hususani kwa Utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (2020-2025) ni matokeo ya umoja, mshikamano na ushirikiano, hivyo ni vyema waendelee kushikama kufanikisha kupatikana kwa mafanikio makubwa zaidi.

Aidha, Kinana amewapongeza Viongozi na Wanachama kwa Ushindi wa Kishindo kufuatia uchaguzi mdogo wa Diwani Kata ya Mahege ambapo mgombea wa CCM Hamada Juma Hingi aliibuka mshindi kwa asilimia 85.

 

Habari Zifananazo

Back to top button