Kinana atunukiwa nishani ya uongozi

MWENYEKITI aliyemaliza muda wa uongozi katika Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), Abdulrahman Kinana, ametunukiwa nishani ya uongozi bora wa kipindi cha mwaka mmoja alipokuwa mwenyekiti wa taasisi hiyo.

Nishani hiyo imekabidhiwa  kwa niaba ya viongozi wakuu wa vyama wanachama wa TCD na Mwenyekiti mpya wa TCD, Profesa Ibrahim Lipumba, katika mkutano wa viongozi wakuu wa vyama wanachama wa TCD, uliofanyika leo Julai 3, 2023, katika ofisi za TCD, Dar es Salaam.

Kabla ya kumkabidhi nishani hiyo, Profesa Lipumba ambaye pia ni Mwenyekiti wa CUF, amesema kuimarika kwa TCD kwa sasa kunatokana na mchango wa kipekee wa Kinana ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi.

“Kwa niaba ya wakuu wenzangu wa vyama vya siasa wanachama wa TCD, uongozi Ndg. Kinana umetuwezesha kutuunganisha sisi wote, tunakukabidhi nishani hii iwe kumbukumbu kwa kazi yako nzuri, asante sana,” amesema Prof. Lipumba.

Viongozi wengine wa vyama vya siasa ambavyo ni wanachama wa TCD waliohudhuria mkutano huo na kushuhudia ni Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, Haji Ambar, Mwenyekiti wa CHAUMMA, Hashim Rungwe, Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo, Juma Duni Haji pamoja na Makatibu wa Kuu wa Vyama hivyo.

Kinana alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa TCD, Aprili mwaka 2022 kwa kipindi cha miezi sita, na baadaye wakuu hao wa vyama walimuongezea muda wa uongozi kwa kipindi kingine cha miezi sita baada ya kufanyika marekebisho ya katiba ya TCD.

Kikao kilimchagua Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, Ambar kuwa Makamu Mwenyekiti wa TCD.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
3 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Kim
Kim
2 months ago

My last paycheck was $2500 for working 12 hours a week online. My sisters friend has been averaging 8k for months now and she works about 30 hours a week. I can’t believe how easy it was once I tried it out. The potential with this is endless.

This is what I do……….>>> https://goodfuture10.blogspot.com

Last edited 2 months ago by Kim
Julia
Julia
2 months ago

Earn income while simply working online. work from home whenever you want. just for maximum 5 hours a day you can make more than $600 per day online. From this i made $18,000 last month in my spare time.
.
.
Detail Here—————————————————————>>>  http://Www.OnlineCash1.Com

Last edited 2 months ago by Julia
Lori L. Kent
Lori L. Kent
2 months ago

I am making easily every month $ 22000 to $ 28000 just by doing simple work from home. This job is online and very easy to do part-time or Full-time even no special experience required for this task. h96 Anyone can now participate in this job and start earning just like me by just click this link….. http://www.pay.hiring9.com

Back to top button
3
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x