Kiongozi upinzani akubali kufanya mazungumzo mtandaoni

MSUMBIJI : KIONGOZI wa upinzani Msumbiji,  Venancio Mondlane amesema atakubali kufanya mazungumzo na Rais Filipe Nyusi kwa njia ya mtandao  au mchakato wa kisheria wa kukamatwa dhidi yake usitishwe.

Rais Filipe Nyusi amemualika Venancio Mondlane ofisini kwake mjini Maputo Novemba 26 baada ya vifo vya watu kadhaa vilivyosababishwa na ukandamizaji wa polisi dhidi ya maandamano ya kupinga matokeo ya uchaguzi Oktoba 9.

Mondlane ambaye ni  mgombea wa kujitegemea amedai kuwa uchaguzi huo ulichakachuliwa ili kukipa ushindi chama cha Frelimo.

Advertisement

Katika hotuba yake  aliyoitoa kwenye ukurasa wa facebook, Mondlane  amesema wako tayari kwa mazungumzo ya kweli na yasiyokuwa na mitego.

Kiongozi huyo wa upinzani amefunguliwa mashtaka ya jinai na kiraia dhidi yake, ikiwemo uharibifu uliosababishwa wakati wa maandamano ya wafuasi wake, ambayo yamepelekea akaunti zake za benki kufungiwa. SOMA: Maandamano yatikisa Msumbiji