MSUMBIJI : VIKOSI vya ulinzi nchini Msumbiji vimefyatua risasi ili kutawanya mamia ya wafuasi wa mgombea urais wa upinzani Venancio Mondlane.
Katika shambulio hilo la risasi vijana watatu wamejeruhiwa kwa risasi huku mmoja akijeruhiwa vibaya.
Mpaka sasa idadi ya watu waliojeruhiwa haijaweza kujulikana licha ya vikosi vya ulinzi na usalama nchini humo kuendelea kuchunguza.
Mondlane na mamia ya wafuasi waliandamana katika mji wa kaskazini mashariki wa Nampula kupinga ushindi wa Frelimo.
Oktoba 9,Chama Tawala cha Frelimo kilishinda uchaguzi katika mkoa wa Nampula kwa asilimia 66 ambapo matokeo yanatarajia kutangazwa Oktoba 24.
SOMA : Uchaguzi Mkuu Msumbiji kufanyika leo