WANACHI wa Msumbiji wanapiga kura leo katika uchaguzi mkuu wa Rais, Bunge la Taifa na mabunge ya majimbo.
Wagombea urais wanne wenye mvuto katika uchuguzi huo ni Daniel Chapo(57) wa FRELIMO, Venancio Mondlane(50)-PODEMOS, Lutero Simango(64)-MDM na Ossufo Momade(63)-MDC.
SOMA: Dola bilioni 5 kuzalisha umeme Msumbiji
Karibu wapiga kura milioni 17 miongoni mwa watu milioni 31 wa nchi hiyo wamekujiandikisha kumchagua Rais mpya pamoja na wabunge 250 wa Taifa na majimbo.
Chama cha Ukombozi Msumbiji cha FRELIMO kimetawala tangu kumalizika kwa ukoloni wa Kireno mwaka1975.
Kwa mara ya kwanza uchauzi huo unahusisha mgombea wa urais aliyezaliwa baada ya uhuru Daniel Chapo, gavana wa jimbo ambaye hakujulikana hadi alipoteuliwa Mei mwaka huu kama mgombea kuchukua nafasi ya Rais anayemaliza muda wake, Filipe Nyusi.
Mpinzani wa jadi wa kisiasa wa FRELIMO ni chama cha RENAMO, kilichoendesha vita ya kiraia kupinga chama tawala iliyodumu toka 1977 hadi 1992 na kusababisha vifo vya watu wanaokadiriwa kufikia milioni moja.