Dola bilioni 5 kuzalisha umeme Msumbiji

MSUMBIJI imesaini mkataba na muungano unaoongozwa na kampuni kubwa ya umeme ya Ufaransa EDF kujenga mradi mpya wa kuzalisha umeme wa Mphanda Nkuwa wenye thamani ya Dola bilioni 5.

Bwawa na kiwanda cha kuzalisha umeme wa maji kitajengwa kando ya mto Zambezi katika jimbo la Tete Kaskazini mwa Msumbiji, na kitazalisha megawati 1,500 za umeme katika awamu ya kwanza.

“Hii ni hatua madhubuti ya kwanza kwa Msumbiji kunufaika na uwezo mkubwa wa kufua umeme wa mto Zambezi na rasilimali nyingine za nishati nchini.” Waziri wa Nishati Msumbiji, Salvador Namburete alisema.

Muungano ulioshinda unaoongozwa na EDF unajumuisha TotalEnergies na Sumitomo Corporation, na utaendeleza, kujenga na kuendesha mradi wa kufua umeme wa Mphanda Nkuwa.

Habari Zifananazo

1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button