Kiongozi upinzani afunguliwa kesi mauaji

MALAWI : KIONGOZI wa chama cha upinzani –UTM nchini Malawi,Patricia Kaliati  amefikishwa mahakamani akituhumiwa kupanga njama za kumuua Rais Lazarus Chakwera.

Kaliati ni Katibu Mkuu wa chama cha UTM, ambaye alikamatwa wiki iliyopita kwa tuhuma za kutaka kumuua Rais Chakwera.

Hapo jana, Mwanasiasa huyo alifikishwa mahakamani na kusomewa shtaka lake huku wenzake wawili hawakuonekana mahakamani.

Advertisement

Hatahivyo, Wakili wa upande wa utetezi amedai mteja wake hana hatia yoyote na kesi hii imeshawishiwa na masuala ya siasa huku wafuasi wa UTM wakiendelea kuipnga serikali kuhusu kesi hiyo.

Upande wa mashtaka nao umejiridhisha kuwa Kaliati na wenzake kweli walipanga njama hizo za kumuua Rais Chakwera.

Hatahivyo,Hakimu anayesikiliza  kesi hiyo amesema Kaliati anahaki ya kupewa dhamana hadi hapo uchunguzi utakapokamilika.

Polisi nchini Malawi wamesema wanafanya kazi kwa mujibu wa sheria na kwamba haki za Kaliati zitaheshimiwa.

SOMA: Malawi waondoa visa kwa nchi 79 duniani