Kiongozi wa upinzani Urusi afariki gerezani

KIONGOZI wa upinzani nchini Urusi Alexei Navalny amefariki dunia akiwa jela, idara ya magereza nchini humo imesema.

Navalny ,47, mmoja wa wakosoaji wakubwa wa Rais Putin, alihukumiwa miaka 19 chini ya “utawala maalum”. Katika video kutoka gerezani mnamo Januari, alionekana amedhoofika.

Ikulu ya Kremlin ilisema haina taarifa kuhusu chanzo cha kifo hicho.

Mapema Desemba alitoweka gerezani ambako alikuwa akitumikia kifungo cha miaka 30 kwa tuhuma za itikadi kali na za ulaghai ambazo aliziita ulipizaji wa kisiasa.

Habari Zifananazo

Back to top button