Kipaumbele kikuu ni afya

ZANZIBAR: MGOMBEA Urais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Chama cha NCCR- Mageuzi, Laila Rajab Khamis ametaja afya kuwa ni kipaumbe kikuu endapo wananchi wa Zanzibar watampa ridhaa ya kuwa Rais wao.

Katika kutekeleza hilo, Laila amesema atawachukua vijana wa Zanzibar na kuwapeleka nje ya nchi kupata ujuzi zaidi ili kuwa na wataalamu wa afya wa kutosha katika kada zote za afya na kuondoa uhaba wa wataalamu hao katika visiwa vya Zanzibar.

“Endapo tume itaniteua kugombea nafasi hii ya Urais wa Zanzibar na wananchi wakanipigia kura ya ndio nikawa Rais wao nitatilia mkazo katika mambo ya maadili, ajira kwa vijana na afya. Kwakuwa sera ya chama chetu ni utu, tutaweka mkazo mkubwa kwenye masuala ya afya”

“Japo hospitali zipo nyingi, hakuna huduma, hakuna wafanyakazi tukiingia madarakani tutachukua vijana wetu, tutawapeleka nje ya nchi)kuwapa elimu na mafunzo watakaporejea kama madaktari bingwa tutawaeneza katika mahospitali yote Unguja na Pemba kila hospitali itakuwa na madaktari bingwa wake, maradhi na madaktari bingwa wake, sio daktari mmoja maradhi yote,”amesema Laila Rajab.

Mgombea huyo ameyasema hayo mara baada Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), Jaji George Kazi kumkabidhi fomu ya kugombea nafasi ya kiti cha Rais kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa Chama cha NCCR-Mageuzi, hafla iliyofanyika katika Afisi za Tume zilizopo Maisara Wilaya ya Mjini Unguja.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button