Kishindo cha Miss Halima Kopwe Tanzania

DAR ES SALAAM: Miss Tanzania aliyewakilisha Tanzania katika shindano la Miss World 2024 Halima Kopwe amerejea Tanzania akitokea nchini India yalikofanyika mashindano ya Miss World mwaka huu.

Miss Halima amefanikiwa kuweka rekodi ya kuingia kwenye orodha ya warembo 40 bora wa mwaka huu katika Miss World kwenye mchujo ambao uliwaacha nje warembo wengine 72 kati ya 112 walioshiriki ambapo mara ya mwisho mwakilishi wa Tanzania kuingia 40 bora ilikuwa ni mwaka 2005 kupitia Nancy Sumari.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati alipowasili Dar es Salaam, Halima amewashukuru Watanzania kwa kumuunga mkono na kumwonyesha ushirikiano bila kuchoka.

“Ushindi ni wa Tanzania nzima na mafanikio mengine niliyoyapata ni project yangu ya “Damu yangu, kizazi changu’ kuingia katika kumi bora ya dunia kati ya project 112 duniani.”

“Nilijitahidi sana kuwekeza kwenye social project hiyo napenda kusema nilivyo-invest kwenye project imelipa na nimepeperusha bendera ya Tanzania kwenye majina yanayotajwa kwenye zile nafasi za Top ‘something’ za Miss Dunia inatambua,.”amesema Halima.

 

 

Habari Zifananazo

Back to top button