Kiswaga: “Safari Mpya ya Maendeleo Kalenga Imeanza”

IRINGA: Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kalenga kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jackson Kiswaga, ameibuka kwa kishindo baada ya kurejesha fomu na kuteuliwa rasmi na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, akiahidi kufanya kampeni za nguvu na za kishindo kusaka kura za Rais, ubunge na udiwani.
Akizungumza mara baada ya kurejesha fomu kwa Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Kalenga, Caroline Otieno, akiwa amesindikizwa na sekretarieti ya CCM Wilaya ya Iringa Vijijini ikiongozwa na Mwenyekiti Costantino Kihwele, Kiswaga alieleza kuwa safari ya maendeleo ya Kalenga bado haijafikia kikomo.
Amesema makubwa zaidi yanakuja endapo yeye na chama chake watapewa ridhaa kuunda serikali ijayo.
Kiswaga aliwataka wananchi wa Kalenga kuendelea kuwa na imani na CCM kwa sababu, kwa miaka mitano iliyopita, jimbo hilo limepiga hatua kubwa katika sekta mbalimbali za kijamii na kiuchumi, na kwamba serikali ijayo itaongeza nguvu mara dufu.

Aidha, Kiswaga amewataka wananchi kumpigia kura Rais Samia Suluhu Hassan katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, 2025, akisema kura kwa Rais ni ishara ya shukrani kwa maendeleo makubwa yaliyopatikana katika jimbo hilo chini ya uongozi wake.
SOMA ZAIDI
Alisisitiza kuwa ushindi wa wagombea wote wa CCM katika ngazi zote utahakikisha kasi ya maendeleo inaendelea, huku akiahidi kufanya kampeni shirikishi zinazojikita katika hoja na mipango ya maendeleo badala ya majibizano.


