KENYA : JAJI wa Mahakama Kuu ya Kenya Chacha Mwita amesema Mahakama Kuu ya Kenya imeruhusu Bunge la Seneti nchini Kenya kuendelea kusikiliza hoja ya kumuondoa madarakani Naibu Rais wa Kenya Rigathi Gachagua.
Gachagua aliwasilisha hoja 26 mahakamani kutaka kusitisha kikao cha Seneti kinachotarajiwa kukaa kesho kujadili kuondolewa kwake madarakani lakini sasa kesi hiyo itawasilishwa katika Bunge la kitaifa kwa ajili ya kusikilizwa.
SOMA ” Majaji Kenya kusikiliza kesi ya Gachagua
Hapo kesho, Naibu Rais wa Kenya Rigathi Gachagua anatarajia kujitetea mbele ya seneti kwa mashtaka yanayomkabili 11 yaliyoidhinishwa na wabunge 282 katika bunge la kitaifa.
Comments are closed.