WAZIRI wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Deogratius Ndejembi amesema kituo cha afya kilichopo kata ya Segese Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama mkoani Shinyanga kianze kufanya kazi kufikia mwezi Novemba.
Kituo hicho kilijengwa kwa fedha za tozo mwaka 2023 kiasi cha Sh milioni 470 baada ya zahanati iliyopo kuelemewa na wagonjwa nakuhitaji kituo cha afya.
Waziri Ndembeji amesema hayo leo Oktoba,6 2024 kwenye ziara maalum ya kukagua miradi ya maendeleo kwa fedha zilizotolewa na Serikali katika Halmashauri ya Msalala nakuambatana na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Annamringi Macha na Mbunge wa Jimbo hilo, Idd Kassimu.
Waziri Ndembeji amemtaka Mganga Mkuu wa Halmashauri hiyo kuanza kutoa huduma za msingi kwa wagonjwa wa nje ili majengo yasiendelee kukaa bure wakati yametumia fedha nyingi kujengwa.
“Weka meza,viti na baadhi ya vipimo vinavyowezekana na ulete mtaalamu kazi ianze mara moja hilo linawezekana sioni sababu zingine,”amesema Ndembeji.
Mbunge Idd Kassimu amesema wamepokea Sh milioni 123 kwaajili ya vifaa tiba na huduma amependekeza inaweza kuanza.
Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Msalala Sist Mosha amesema bado jengo la mama na mtoto halijakamilika na changamoto nyingine hakuna huduma ya maji na nishati ya umeme.
Comments are closed.