Kituo chaahidi huduma bora

DAR ES SALAAM: WANANCHI wameendelea kunufaika na ajira katika cha Kituo Uwekezaji cha APC Hotel and Conference Centre huku kituo kikijivunia huduma bora kwa wananchi wake.
Kituo hicho kimesema kitaendelea kikijipambanua kwa huduma zake zinazokidhi viwango vya kimataifa. Huduma hizo zimechangia kukuza uchumi na kuvutia wawekezaji kutoka ndani na nje ya nchi, hususan katika sekta ya biashara na utalii.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Ofisa Masoko wa kituo hicho, Happy Sanga, amesema kituo hicho kinaendelea kushirikiana na serikali katika kuboresha ubora wa huduma ili kuvutia wawekezaji zaidi. Amesema juhudi hizo pia zimekuwa kichocheo cha ajira kwa wananchi na kuongeza idadi ya wateja wanaotumia huduma zao.



