Kivumbi ‘Derby’ ya Madrid mtoano UCL leo
MICHEZO minne ya kwanza ya mtoano timu 16 bora Ligi ya Mabingwa Ulaya (UCL) inaanza leo ukiwemo wa ‘derby’ ya Madrid, Hispania kati mabingwa watetezi Real Madrid na Atletico Madrid.
Mchezo huo utapigwa kwenye uwanja wa Santiago Bernabeu jijini Madrid.
Kwa mara ya mwisho zilipokutana katika mchezo wa Ligi Kuu Hispania (LaLiga) Februari 8, 2025 kwenye uwanja huo timu hizo zilitoka sare ya 1-1.
Katika michezo mingine leo, Arsenal itakuwa ugenini kwenye uwanja wa Philips uliopo jiji la Eindhoven, Uholanzi kuikabili PSV Eindhoven.
Borussia Dortmund wa Ujerumani itakuwa wenyeji wa Lille ya Ufaransa kwenye uwanja wa Signal Iduna jijini Dortmund.
Nayo Aston Ville ya England itakuwa ugenini kuikabili Club Brugge ya Ubelgiji kwenye uwanja wa Jan Breydel uliopo mji wa Bruges.



