Kocha Poland atimuliwa baada ya mechi sita
KOCHA Fernando Santos ametimuliwa kuifundisha timu ya taifa ya Poland ikiwa ni mwaka mmoja tangu aichukue timu hiyo.
Santos alitimuliwa timu ya taifa ya Ureno mwaka jana baada ya kuwa na mwenendo usioridhisha akiwa na taifa hilo.
Kocha huyo ameiongoza Poland mechi sita tu tangu aichukue timu hiyo.
Imeelezwa kusuasua na matokeo yasiyoridhisha yamemuondoa kocha huyo Poland.