Kocha Simba ataka mashine mpya 5

KOCHA wa Simba, Roberto Oliveira ‘Robertinho’, amesema ili timu hiyo irudi kwenye ushindani wa kuwania mataji na watani zao Yanga, wanapaswa kusajili wachezaji watano wapya wenye viwango vya kimataifa.

Akizungumza na HabariLEO, kocha huyo amesema kikwazo kikubwa kilichoigarimu timu hiyo kushindwa kufanya vizuri kwenye mashindano ya ndani na nje ni kukosa wachezaji wenye ubora na uzoefu mkubwa kama ilivyokuwa kwa timu nyingine walizokutana nazo kwenye mashindano ya kimataifa.

“Kama nitapata wachezaji watano wapya katika nafasi za ushambuliaji, kiungo mkabaji, beki wa kati, winga na beki wa pembeni mmoja naamini msimu ujao Simba itabeba ubingwa wa mataji yote ya ndani na tutafika mbali kwenye michuano ya kimataifa,”amesema Robertinho.

Simba endapo itamaliza msimu huu bila ubingwa, itakuwa imekamilisha misimu miwili bila kubeba taji lolote ndani na nje ya Tanzania.

Habari Zifananazo

1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button