Kocha Yanga aingia na mkakati mpya dhidi ya Mashujaa

KIKOSI cha Yanga kinachonolewa na Kocha Mkuu Hamdi Miloud kinashuka dimbani Februari 23 kusaka alama tatu muhimu katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Mashujaa mkoani Kigoma.

Yanga itakuwa ugenini katika mchezo huo katika dimba la Lake Tanganyika, mkoani humo kila timu ikihitaji alama tatu ili kufikia malengo yake, huku wananchi ikitaka kuendelea kujiimarisha katika uongozi wa ligi hiyowakati Mashujaa ikihitaji kujiweka salama kutoshuka daraja.

Wachezaji wa kikosi cha Yanga wakifanya mazoezi hivi karibuni kabla ya kusafiri kwenda Kigoma.

Kuelekea mchezo huo kocha wa Yanga, Miloud amesema wanawaheshimu wapinzani wao kwani ina uwezo wa kucheza vizuri, ina wachezaji wengi wazuri na anafikiri inaweza kuwa juu zaidi kwenye msimamo wa ligi na kwamba anajua kila timu inataka kufanya kila kitu kushida dhidi timu yake.

Sehemu ya mashabiki wa Yanga wakiipokea timu yao baada ya kuwasili mkoani Kigoma.

“Wachezaji wetu wanajua hilo, tunapaswa kufanya kila kitu kutumia jitihada nyingi kushinda mchezo huu. Ni jambo jema kuwa na siku tano kabla ya mchezo huu, nafasi nzuri kwangu kuelewa wachezaji wangu vizuri zaidi,” amesema.

Miloud amesema amepata muda wa kufanya marekebisho ya kiufundi mazoezini, kuweka mtazamano wake kidogo kwa sababu si rahisi kubadilisha kila kitu mara moja kwani wachezaji wana tabia zao za uchezaji na kwamba sio rahisi kubadilisha kila kitu.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button