DAR ES SALAAM: WAZIRI wa Ardhi, Miundombinu, Uchukuzi na Utalii wa Japan, Konosuke Kokuba anatarajia kufanya ziara ya kikazi nchini mwezi Januari 2024 kujadili fursa mbalimbali zinazotokana na ushirikiano kati ya Tanzania na Japan katika maendeleo ya miundombinu.
Katika ziara hiyo, Kokuba ataongozana na ujumbe wa watu 40 kutoka kampuni binafsi zinazojihusisha na masuala ya miundombinu na baadhi ya watumishi wa Wizara yake.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Prof. Godius Kahyarara amesema katika kikao cha pamoja cha maandalizi ya ziara hiyo kilichoshirikisha viongozi wa Wizara ya Uchukuzi na Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Plasduce Mbossa jijini Dar es Salaam
Kwa upande wa Japan, ujumbe wake uliongozwa na Yoshihiro Kakishita kutoka Sekretarieti ya Wizara ya Ardhi, Miundombinu, Uchukuzi na Utalii ya Japan.
Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Plasduce Mbosaa ametumia fursa hiyo kuwakaribisha wafanyabiashara na wawekezaji kutoka Japan kuja kuwekeza kwa upande wa miundombinu ya Bandari nchini.
Comments are closed.