Kongamano la kimataifa la muziki kufanyika Dar

DAR ES SALAAM: KONGAMANO la kimataifa la muziki la ACCES limepangwa kufanyika Novemba 9 hadi 11 jijini Dar es Salaam.

Kongamano hilo litahudhuriwa na wasanii wa muziki kutoka ndani na nje ya nchi lina lengo la kudumisha ushirikiano.

Akizungumza leo Oktoba 6,2023 jijini Dar es Salaam, Mratibu wa kongamano hilo Dotto Kahindi kutoka Music In Africa Foundation, amesema mbali na wanamuziki kutoka mataifa mbalimbali kutumbuiza pia kutakuwa na watoa mada zaidi ya 40 kutoka Afrika na duniani kote, ambao wataangazia mambo muhimu kwenye tasnia ya muziki kitaifa na kimataifa, na namna ya kuukuza, kukuza ujuzi na fursa kwa wadau katika tasnia ya muziki Afrika.

Amesema kongamano hilo linafanyika kila mwaka kwenye miji mbalimbali ndani ya Afrika, na kutoa fursa kwa wanamuziki kukuza na kujenge uwezo wao na kutumbuiza mbele ya hadhira iliyosheheni wageni wa kitaifa na kimataifa, ikiwemo waandaaji wa matamasha, mapromota, mawakala wa muziki, lebo za kurekodi muziki na hadhira yenye ushawishi mkubwa.

“Pia wageni watapata fursa ya kutembelea vituo mbalimbali vya tasnia ya muziki Tanzania,”amesema.

Amesema kongamano hilo ni bure kwa Waafrika ambao watataka kushiriki na ili upate nafasi ya kuhudhuria wanatakiwa kujisajili kwanza kupitia tovuti rasmi.

Miongoni mwa watu mashuhuri wataoshiirki kwenye kongamano hilo nimwanamuziki na mjasiriamali wa Afrika Kusini Sho Madjozi atakayefanya mahojiano na Heather Maxwell wa Sauti ya Amerika, wakati msanii na
mtayarishaji wa muziki wa bongo flava kutoka Tanzania Marioo atatoa mada kwenye mkutano huo.

Amesema, ACCES pia itaandaa mijadala ya kina kuhusu usimamizi wa haki za muziki, ujasiriamali wa muziki, uchapishaji wa muziki, branding, ziara za muziki, ushirikiano na teknolojia katika tasnia ya muziki.

Baadhi ya wazungumzaji mashuhuri ni pamoja na mwanzilishi wa SymphonyoS Chuka Chase (Marekani), mwanzilishi wa Roxanne Sonia Boton-Gboh (Ufaransa), Ofisa Maendeleo wa kimataifa wa SACEM Afrika Akotchayé Okio (Ufaransa) na Mkurugenzi Mkuu wa Sony Music Publishing Afrika Kusini, Rowlin Naicker (AfrikaKusini).

Wengine ni mwanzilishi wa Singeli Festi, Masudi Kandoro (Tanzania), Mwanzilishi wa SaveFi Tech Ebenezer Akachukwu (Nigeria), Mwanzilishi Mwenza wa Vth Season, Raphael Benza (Afrika Kusini), Mwanzilishi wa SlikourOnLife, Siya Metane (Afrika Kusini) na Meneja Mkuu EMPIRE, Moody Jones (Marekani).

Amesema mbali na biashara ya muziki kuwa ngumu, ACCES itaitazama zaidi singeli, sauti ya elektroni ya Kitanzania inayoisumbua dunia, kwa kuandaa jopo la majadiliano mahususi kuhusu aina hiyo ya muziki ambapo wakali wa muziki huo wa singeli Balaa MC na Kadilida watashiriki kwenye majadiliano hayo, pamoja na live performances kila jioni.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x