KOREA KUSINI : Mahakama yaruhusu Yoon Suk akamatwe

KOREA KUSINI : MAHAKAMA nchini Korea Kusini imeidhinisha hati ya kukamatwa kwa Rais Yoon Suk Yeol, ambaye alishtakiwa bungeni na kusimamishwa kazi.

Ofisi ya uchunguzi wa ufisadi kwa viongozi wa juu imethibitisha kuwa Mahakama ya Wilaya ya Seoul Magharibi iliidhinisha hati iliyoombwa na maafisa wanaochunguza hatua aliyoichukua Rais Yoon kutangaza hali ya tahadhari nchini humo.

Hii itakuwa mara ya kwanza kutolewa kwa hati ya kukamatwa nchini humo dhidi ya rais aliyeko madarakani.

Hadi sasa bado haijabainishwa ni lini au ni vipi hati ya kukamatwa kwa Yoon itatekelezwa. Hatahivyo, SOMA: KOREA KUSINI : Rais Yoon Suk avunja ukimya

Idara ya Usalama wa Rais ya Korea Kusini imesema itahakikisha hati hiyo ya kukamatwa kwa Rais Yoon inatekelezwa kwa mujibu wa sheria.

Mmoja wa mawakili wake amesema kuwa waranti hiyo imetolewa kinyume cha sheria na batili, na taasisi hiyo haina mamlaka ya kufanya uchunguzi huo.

 

Habari Zifananazo

Back to top button