KOREA KUSINI : RAIS wa Korea Kusini Yoon Suk Yeol amesema uamuzi wake wa kushtukiza wa kutangaza hali ya hatari nchini humo ni kutaka kulinda demokrasia ya nchi hiyo.
Katika hotuba ambayo haikutarajiwa kutangazwa, Rais Yoon Suk amesema tangazo hilo la hali ya hatari lilifanyika kisheria ili kuzuia kuporomoka kwa demokrasia nchini humo na kuwadhibiti wabunge wa upinzani ambao lengo lao kuvunja amani ya nchi.
“Nitasimama kidete iwapo nitashtakiwa au kuchunguzwa,” alisema.
Aliongezea kuwa,”Nitapigana hadi mwisho”.Alimalizia.
SOMA: Chama tawala kimemtaka Yoon Suk kujiuzulu
Kwa sasa, Rais Yoon Suk na washirika wake wanakabiliwa na mashtaka ya uasi ambao wote wamepigwa marufuku kusafiri nje ya nchi hadi uchunguzi utakapokamilika.
Wakatihuohuo, Rais Yoon Suk ameahidi kuendelea kutimiza majukumu yake kama Rais wa Korea Kusini na majukumu mengine ya kisiasa ili kustawisha maendeleo ya nchi hiyo.