Korea yabusti elimu ya Tehama nchini

DAR ES SALAAM: UJIO wa mradi wa “Korea e- learning Improvement Cooperation (KLIC) utasaidia kuboresha elimu nchini katika eneo la TEHAMA.

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), Dk. Aneth Komba amesema hayo leo Novemba 6, 2023 alipoambatana na Gavana wa Gwangju Metropolitan, Lee Jeong na Wataalamu wengine kutoka Korea Kusini wakikagua mradi huo katika shule ya msingi Tegeta A Jijini ,Dar es Salaam.

Amesema, mradi huo umekuja kwa wakati muafaka ambapo Serikali tayari imetangaza Sera mpya ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 toleo la 2023 ambapo kuanzia mwaka 2024 mtaala mpya unatarajiwa kuanza kutumika.

Kwa upande wake, Gavana wa Gwangju Metropolitan, Lee Jeong ameishukuru Serikali kupitia TET kwa kusimamia vizuri mradi huo na kuhakikisha wanafunzi wananufaika.

Amesema, Gwangju itaendelea kuisaidia Tanzania hasa katika eneo la TEHAMA ili kuongeza kasi ya maendeleo kupitia elimu.

Habari Zifananazo

Back to top button