Korosho tani 20,000 kupelekwa mnadani

Korosho tani 20,000 kupelekwa mnadani

TANI 20,000 za korosho ghafi zinatarajiwa kupelekwa kwenye mnada wa pili msimu wa mauzo 2022/2023, ambao unaanza leo sehemu mbalimbali nchini.

Kaimu Mkurungezi wa wa Bodi ya Korosho nchini (CBT), Alfred Francis amesema minada hiyo ya pili itaanza leo na kumalizika tarehe 3 Novemba mwaka huu.

Francis amesema korosho hizo ni pamoja na zile tani 15,000 ambazo hazikuuzwa kwenye mnada wa kwanza Oktoba 22 katika mikoa ya Lindi na Mtwara.

Advertisement

Wakulima wa korosho katika mikoa ya Lindi na Mtwara walikataa kuuza korosho hizo kwa madai kuwa bei iliyotangazwa na wanunuzi ni ndogo kuliko uzalishaji.

Katika Minada hiyo ambayo ilifanywa na vyama vya vikuu vya ushirika vya TANECU, MAMCU, RUNALI na Lindi Mwambao, bei ya juu ya korosho Kwa kilo ilikuwa Sh 2,200 na bei ya chini ilikuwa Sh 1,480.

Hata hivyo wakulima walidai bei hiyo haina maslahi, hivyo kukataa kuuza korosho ambazo zilirudishwa kwenye maghala zikisubiria mnada mwingine.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *