DAR ES SALAAM; UCHANGANYAJI wa kuku tofauti kwenye banda moja, unafifisha uwezo wa asili, jambo linalosababisha watu wengi kushindwa kwenye biashara ya kuku.
Akizungumza na HabariLEO, mwanzilishi wa Taasisi ya EKNO Group, Ebenezer Lema amesema baadhi ya wafugaji hawafahamu kuhusu taratibu hizo badala yake wanachanganya kuku eneo moja.
“Kuku mmoja anapokuwa vizuri kwenye utagaji wa mayai na mwingine kwenye nyama, unapowachanganya wanafifisha uwezo wa asili wa kuku wa mayai na huyo wa nyama.
Soma: Wafugaji kuku Dar wawatwisha lawama wafanyabiashara
“Tunahamasisha wafugaji kufuga kuku kutokana na aina, unafuga kiasili kwa kuwa na aina moja ya kuku,” amesema.
Pia ameelezea changamoto nyingine inayowakuta wafugaji wa kuku asili, ni kuwapa dawa za kisasa na kuwatibu kwa muda mrefu.
Amesema kuhusu hilo la dawa, wamekuja na muundo wa tiba ambayo ikitumiwa vizuri hakuna haja ya kutumia dawa.
Soma: Kuku waadimika msimu wa sikukuu
“Hapa tunashauri sana kwa sababu katika kinga unatumia muda mchache lakini hata gharama unazotumia inakuwa ni ndogo ukilinganisha na zile za kisasa. Kwa kifupi tumeunda utaratibu wa kuwapa kinga vifaranga na kuku wakubwa,” amesema.
View this post on Instagram
Ametaja magonjwa yanayosumbua kuku ni taifodi, mafua, kuhara damu, kideri na ndui na kueleza kuwa gharama kubwa ya chakula cha kuku imekuwa ikirudisha nyuma wafugaji, hivyo wao wanahamasisha wafugaji kutumia chakula kitwacho azola.
Anasema chakula hicho azola kinaoteshwa kwenye maji, ni mmea aina ya magugu hauna gharama kwa mfugaji.