Kuna shida watoto Kusuka?

DAR ES SALAAM: Imekuwa ni jambo la kawaida katika jamii zetu kwa sasa, kuona hata watoto wadogo wakiwa katika mitindo mbalimbali ya nywele kichwani bila kujali umri wa watoto wenyewe, je kuna usahihi katika hili?

Sio mbaya mtoto kupendeza, lakini unapaswa kuangalia aina ya urembo na mapambo unayomwekea.

Kusuka kwa watoto si tatizo kama atakuwa amefikisha umri fulani, lakini tatizo la wazazi unakuta anamsuka mtoto wa miaka miwili au mwaka mmoja bila kujali kama utosi ama ngozi ya kichwa haijakomaa.

Wazazi wamekuwa na tabia za kuwasuka watoto wa kike ama kwa hiari au kwa kuwalazimisha, lengo ni kuwapendezesha kimwonekano.

Hakuna kipindi ambacho watoto wanaumia kama msimu ambao wazazi wanalazimisha mtoto asuke mtindo ambao unakuwa mgumu, mara nyingi inakuwa mitindo inayosukwa sana na watu wazima.

Pamoja na kupata maumivu, pia unamfanya mtoto atumie muda mrefu kukaa.

Siyo vizuri kuiga kila tunaloona bila kufuatilia na kubaini athari zinazoweza kutokea, kabla ya kutumia kitu ni vizuri kufanya utafiti na uamuzi wa kukitumia au kukiacha kifanywe baada ya kupima faida na hasara zake.

Si mbaya mtoto kupendeza, lakini unapaswa kuangalia aina ya urembo na mapambo unayomweka.

Kusuka kwa watoto si tatizo kama atakuwa amefikisha umri fulani, lakini tatizo la wazazi unakuta anamsuka mtoto wa miaka miwili au mwaka mmoja bila kujali kama utosi ama ngozi ya kichwa haijakomaa.

Unaweza kumsuka mtoto lakini si lazima umsuke nywele ambazo zitamletea maumivu.

Ukienda kwenye saluni za watoto utakuta mzazi kakaa anamsimamia mtoto anasuka huku analia, lakini anamlazimisha mpaka amalize bila kujali kama anaumia.

Si sawa kufanya hivyo, wazazi wanapaswa kufahamu kuwa kusuka kunaenda sambamba na kuvuta ngozi ya kichwa na kusababisha maumivu endapo utakuwa na ngozi laini.

Si kuumiza ngozi tu, kuna nywele nyingine unasuka hata mtu mzima unasikia mpaka mishipa ya kichwa inauma. Je, kwa watoto unadhani maumivu yake yanakuwaje?

Maumivu yote unayoyahisi mtu mzima unadhani mtoto anaweza kuvumilia hali hiyo, kwani mtoto asiposuka atapungukiwa nini.

Kama mmeshachunguza watoto wanaoanza kusukwa nywele mapema sura zao huwa zinaonekana kukomaa na baadhi yao mwonekano wanaokuwa nao hauendani na umri wao.

Kwa kuzingatia hilo, mzazi unatakiwa kuanza kumsuka mtoto akiwa na angalau miaka mitano.

Miaka mitano mtoto anakuwa ameshakomaa utosi na kama utaweza bora uwe na utaratibu wa kumkata nywele mpaka atakapokuwa mkubwa, muda ambao atakuwa anajiamulia mambo yake mwenyewe.

Siamini kama urembo wa nywele kwa mtoto ni wa kuzingatia, kwakuwa kwanza katika kipindi hicho anakuwa bado hajajua maana ya urembo.

Kuna watoto wengi tunawaona wanakata nywele na wanavalishwa vizuri bado wanapendeza na kuonekana warembo, wazazi wanapaswa kuwa makini katika vitu ambavyo si vya lazima.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
3 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
EmmaJames
EmmaJames
21 days ago

My last salary was $8,750 only worked 12 hours a week. My longtime neighbor estimated $15,000 and works about 20 hours for seven days. I can’t believe how blunt he was when I looked up his information.
.
.
Detail Here——————————————————>>>  http://Www.BizWork1.Com

Angila
Angila
21 days ago

Making every month extra dollars by doing an easy job Online. Last month i have earned and received $18539 from this home based job just by giving this only mine 2 hrs a day. Easy to do work even a child can get this and start making money Online. Get this today by follow instructions……
.
.
.
On This Website……………..> > W­w­w.S­m­a­r­t­c­a­r­e­e­r­1.c­o­m

Terrieuggan
Terrieuggan
21 days ago

I’ve gained only within four weeks by comfortably working part-time from home. Immediately when I had lost my last business, mtg I was very troubled and thankfully
following website___________ http://Www.Careers12.com

Last edited 21 days ago by Terrieuggan
Back to top button
3
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x