SUDAN : TAKRIBAN watu 13 wameuawa kwa kupigwa risasi katika shambulizi linalodaiwa kufanywa na kundi la wanamgambo la RSF katika jimbo la Al-Jazira kusini mwa Khartoum nchini Sudan.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa nchini humo imesema kuwa kundi la wanamgambo la RSF liliwafyatulia risasi watu hao waliokuwa katika mji wa Al-Hilaliya.
Jimbo la Al-Jazira nchini Sudan limeendelea kuwa ni kitovu cha mapigano tangu kamanda wa RSF, Abu Aqla Kaykal, alipotangaza kuliasi kundi hilo na kujiunga na upande hasimu wa jeshi la taifa.
Naye Mratibu wa utoaji wa misaada ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan, Clementine Nkweta-Salami amesema kundi la wanamgambo RSF lilianzisha mashambulizi katika maeneo ya mashariki ya jimbo la Al-Jazira tangu Oktoba 20 hadi 25.
Hatahivyo , amesema wanamgambo hao wanatuhumiwa pia kufanya mauaji ya halaiki, vitendo vya unyanyasaji watu kingono, uporaji mali kwenye masoko na majumba pamoja na kuchoma moto mashamba.
SOMA : Guterres aonya kuhusu sudan