YEMEN : WAASI wa Houthi nchini Yemen wametishia kufanya mashambulizi zaidi dhidi ya Israel ikiwa nchi hiyo haitaheshimu makubaliano ya kusitisha mapigano Gaza.
Katika hotuba yake,kiongozi wa kundi hilo Abdul-Malik al-Houthi amesema mafanikio yaliyofikiwa katika mazungumzo kati ya Israel na Hamas ni maendeleo muhimu na kwamba kundi hilo linafuatilia kwa karibu utekelezaji wake. SOMA: Waasi washambulia meli Yemen
Al-Houthi ameongeza kuwa wanamgambo hao wako tayari kutoa msaada wa kijeshi kwa Wapalestina ikiwa kutashuhudiwa ukiukwaji au mashambulizi ya Israel.
Waasi wa Kihouthi wamekuwa wakikabiliana na Israel kwa zaidi ya mwaka mmoja ili kudhihirisha uungwaji wao mkono kwa Wapalestina katika vita vya Gaza.