Kwata kupigwa Lake Tanganyika leo

Sehemu ya wachezaji wa Mashujaa wakifanya mazoezi

LIGI Kuu Tanzania Bara inaendelea leo kwa mchezo mmoja kwenye uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma.

Wenyeji Mashujaa itakuwa nyumbani kaikarisha Tanzania Prisons.

SOMA: Mashujaa wazindukia kwa KMC

Advertisement

Mashujaa ipo nafasi 3 katika msimamo Ligi Kuu ikiwa na pointi 3 baada ya mchezo 1 wakati Tanzania Prisons inashika nafasi ya 5 ikiwa na pointi 1.

Katika mchezo wa mwisho wa Ligi timu hizo kukutana Mei 20, Mashujaa ilishinda kwa 2-1.