Lampard kocha mpya Chelsea

RASMI: Chelsea imemteua Frank Lampard kuwa kocha mkuu wa timu hiyo mpaka mwisho wa msimu, akichukuwa nafasi ya Graham Potter aliyetimuliwa mwanzoni mwa wiki hii.
Taarifa zinaeleza kuwa klabu hiyo itaendelea kuwatafuta makocha wengine ambao watachukuwa nafasi ya Lampard msimu utakapoisha.
Ikumbukwe mwaka 2019 Chelsea iliwahi kumpa ajila Lampard ya kuwa kocha mkuu na mwaka 2021 ikamtimua kutokana na matokeo mabovu.
Baada ya hapo 2022, Lampard alitapa nafasi ya kuifundisha Everton, mwanzoni mwa msimu huu alitumuliwa kutokana na matokeo yasiyoridhisha.



