Wabunge wa Latvia wajiondoa katika mkataba wa mabomu ya ardhi

LATVIA : WABUNGE nchini Latvia wameamua kuchukua hatua muhimu  ya kupiga kura  ya kuiondoa nchi hiyo kwenye mkataba wa kupiga marufuku matumizi ya mabomu ya ardhini.

Hatua hii inakuja wakati nchi hiyo inayopakana na Urusi, ikikabiliwa na hali ya wasiwasi kutokana na vita vinavyoendelea nchini Ukraine.

Uamuzi huu unalenga kuimarisha usalama wa Latvia, ambayo ni mwanachama wa Umoja wa Ulaya na Jumuiya ya kujihami ya NATO.

Tangu Urusi ilipofanya uvamizi wa Ukraine mwaka 2022, Latvia pamoja na mataifa mengine katika ukanda huu, wamekuwa wakiongeza bajeti zao za ulinzi na kutoa mafunzo ya kijeshi kwa ajili ya kukabiliana na vitisho vinavyoweza kutokea.

Mkataba wa Ottawa, ambao unakataza matumizi ya mabomu ya ardhini, umetiwa saini na nchi 160, ingawa Marekani na Urusi hazijama katika kundi hilo. Kutokana na hofu ya kushambuliwa na Urusi, nchi za Baltic zimejizatiti kushirikiana zaidi katika masuala ya usalama wa kikanda.

SOMA:  Finland kujiunga Nato

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button