Leo tena kinapigwa Ligi kuu Tanzania bara

MZUNGUKO wa 14 wa Ligi kuu Tanzania bara utaendelea leo ambapo wajelajela Tanzania Prisons watakuwa Uwanja wa Sokoine Mbeya wakiminyana na Namungo Fc kuanzia saa 8:00 mchana.
Prisons wanaingia katika mchezo huo wakiwa nafasi ya 11 na alama zao 14 huku Namungo wakivimba na alama 17 katika nafasi ya nane.
Mchezo mwingine wa ligi hiyo matajiri wa dhahabu, Geita Gold watawavaa walima alizeti wa Singida Fc kuanzia saa 10:00 jioni , huku mchezo wa mwisho kwa siku ya leo vinara wa ligi hiyo, Azam Fc wakiwa ugenini dhidi ya Kagera Sugar kuanzia saa 1:00 usiku.

Habari Zifananazo

Back to top button